Huwezi kusikiliza tena

Upinzani wakataa matokeo Msumbiji

Raia wa Msumbiji walipiga kura kumchagua rais mpya na vile vile wabunge. Chama cha Frelimo, ambacho kimeiongoza nchi hiyo tangu ilipojinyakulia uhuru mwaka 1975, kimeshindana na chama cha upinzani, Renamo.

Kulingana na matokeo chama tawala kimeshinda uchaguzi huo ingawa upinzani Renamo unasema haukubali matokeo hayo ya uchaguzi uliofanyika Jumatano. Ulikuwa uchaguzi wa Rais na wabunge.

Msemaji wa Renamo anasema kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya udagngayifu huku wpaiga kura wakitishwa.

Kiongozi wa Renamo, Afonso Dhlakama, alijitokeza kutoka mafichoni mwezi uliopita, na kuamua kuwania urais, baada ya mapatano ya amani kati ya chama chake na serikali.

Mgombea wa chama kilicho madarakani ni Filipe Nyusi, aliyekuwa wakati mmoja waziri wa ulinzi.

Mwandishi wa BBC Immanuel Igunza yuko mjini Maputo.