Huwezi kusikiliza tena

Ebola yaacha watoto bila wazazi

Shirika la afya duniani limetangaza rasmi kuwa taifa la Nigeria halina ugonjwa wa Ebola, wiki sita baada ya kutoripotiwa kwa visa vya ugonjwa huo .

Nchi giyo yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, lipokea sifa tele kwa hatua zake za haraka kukabiliana na Ebola baada ya mwanmadiplomasia Mliberia mwenye ugonjwa huo kwenda Nigeria mwezi Julai.

Ugonjwa huo umekuwa janga kubwa nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone, ambako zaidi ya watoto 4,000 wameachwa bila wazaziwaliofariki kutokana nao.

Shirika la misaada la Uingereza Street Child, limezungumza na watu nchini Sierra Leone ambao wamethiriwa na ugonjwa huo.