Ulaji nyama ya nguruwe una madhara
Huwezi kusikiliza tena

Je nyama ya Nguruwe ina madhara?

Image caption Ulaji nguruwe

Kumekuwa na mjadala mkali kuhusu uhalali wa kula nyama ya nguruwe katika maeneo mengi duniani huku wataalam wa lishe, afya na wanyama wakitofautiana kuhusu madhara ya kula mnyama huyo.

Juma lililopita Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza alitembelea mji wa Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo alifanya mazungumzo na mtu mmoja ambaye amekuwa anakula nyama ya Nguruwe kwa miaka 40 sasa.