Waziri Pinda atangaza kuwa
Huwezi kusikiliza tena

Mizengo Pinda kuwania Urais Tanzania

Waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, ametangaza niya yake ya kuwania urais katika uchaguzi ujao .

Pinda aliyasema hayo mjini London ambako mkutano wa viongozi unaoangazia uwekezaji zaidi katika bara la Afrika unaendelea .

Viongozi hao wanatumaini kuyashawishi mashirika makubwa zaidi ya uwekezaji, katika mkutano huo wa siku mbili, kwamba yanafaa kuwekeza zaidi katika mataifa ya Afrika, hasa Nigeria, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ghana na Togo.

Waziri mkuu Mizengo Pinda alitutembelea hapa BBC mjini London na kuzungumza na televisheni ya DIRA YA DUNIA.