Rais wa Zambia Michael Sata aaga dunia
Huwezi kusikiliza tena

Rais wa Zambia Michael Sata aaga dunia

Rais wa Zambia Michael Sata amefariki akiwa na umri wa miaka 77 baada ya kupata matibabu ya ugonjwa usiojulikana . Kulingana na serikali, Sata ambaye alikuwa akitibiwa nchini Uingereza,alifariki katika hospitali ya King Edward wa saba siku ya jumaane usiku.

Vyombo vya habari vinasema kuwa alifariki ghafla kutokana na shinikizo la moyo.

Kifo cha rais huyo kinajiri baada ya Zambia kusherehekea miaka hamsini ya maadhimisho ya uhuru wao kutoka Uingereza.

Ni Kiongozi wa pili wa Zambia kufariki akiwa afisini baada ya Levy Mwanawasa mnamo mwaka 2008.