Watoto waliosajiliwa jeshini
Huwezi kusikiliza tena

Watoto wasajiliwa wanajeshi Sudan Kusini

Mazungumzo ya upatanishi yakiwa yanaendelea kati ya Rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar, hali ya maisha ya kawaida nchini Sudan Kusini bado ni ya kusuasua. Nchi hiyo iliyopata uhuru wake mwaka 2011, imekuwa katika mzozo wa wenyewe kwa wenyewe uliosababisha watu wengi kukimbia makazi yao. Wakati huohuo watoto wapatao elfu kumi na moja wamechukuliwa kupigana katika makundi yenye silaha nchini humo, likiwemo jeshi la serikali. Mariam Dodo Abdallah ametuandalia taarifa hii.