Ebola :CAF yakataa kuahirisha kombe la Afrika
Huwezi kusikiliza tena

CAF yakataa kuahirisha kombe la Afrika

Shirikisho la kandanda barani Afrika - CAF, linataka maandalizi ya kombe hilo yafanyike jinsi yalivyopangwa kati ya mwezi Januari na Februari mwaka ujao.

Caf imekatalia mbali ombi la Morocco kutaka mashindano yahairishwe kutoka na hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu nne na mia nane.

Aidha, CAF imeomba mataifa saba barani Afrika iwapo watakuwa radhi kuandaa mashindano ya kombe hilo.

Kufikia sasa hakuna taifa ambalo limekubali kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Morocco ilikuwa imeomba kuahirishwa kwa mashindano hayo hadi mwezi Juni mwakani.