Mradi wa kopa ng'ombe lipa ng'ombe TZ
Huwezi kusikiliza tena

Mradi wa kopa ng'ombe lipa ng'ombe TZ

Wanawake zaidi ya 180 wafugaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki hatimae wameweza kujitegemea kiuchumi, na kuendesha biashara ndogo ndogo.

Hii ni baada ya wanawake hao kuwezeshwa katika mradi wa kopa ng'ombe lipa ng'ombe, unaombatana na mafunzo ya kitaalamu ya kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa ufanisi zaidi.

Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau alikutana na baadhi ya wanawake hao katika mkoa wa Njombe na kutuandalia taarifa ifuatayo.