Waombolezaji wa Kulipwa nchini Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Waombolezaji wa Kulipwa Kenya

Kila Alhamisi na Ijumaa, shughuli nyingi katika mji wa Kisumu, ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Kenya, husimama kwa muda.

Mamia ya pikipiki au (Bodaboda), husababisha msongamano katika barabara za mji.

Kwa nini? Wao huwa ni waombolezaji wa kulipwa.

Kadri msafara ulivyo mrefu, na kelele za waombolezaji kuzidi, ndivyo marehemu hufahamika kuwa ni mtu maarufu.

Dennis Okari anaarifu kutoka Kisumu.