waombolezaji
Huwezi kusikiliza tena

Je,wajua kuna waombolezaji wa kulipwa ?

Kila Alhamisi na Ijumaa, shughuli katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya, huvurugika kwa sababu mamia ya waendesha pikipiki huzuia barabara kutokana na kukodiwa kuomboleza msiba kwa malipo.

Kelele za sauti zao, ukubwa wa misafara ya pikipiki vinatumiwa kama kigezo cha umaarufu na heshima kwa marehemu.

Lakini sasa haya yote huenda yakawa mambo ya kale, baada ya serikali ya kaunti ya Kisumu kuharamisha mtindo huu wa uombolezaji. Mwandishi wetu Dennis Okari anaarifu zaidi.