Huwezi kusikiliza tena

Umri wamvua Miss Tanzania Taji

Miss Tanzania Sitti Mtemvu amejivua taji la Miss Tanzania aliloshinda mwaka huu mjini Dar es Salaam baada ya kuzongwa na mashabiki kuhusu umri wake.

Akizungumza na BBC Mkurugenzi wa Lino International Agency Hashim Lundenga waandaji wa shindano la Miss Tanzania amesema kuwa mrembo huyo amejivua mwenyewe taji hilo kwa kuandika barua bila kushinikizwa na mtu yeyote.