roboti
Huwezi kusikiliza tena

Roboti kuchukua kazi za raia Uingereza

Sio raia wa Australia pekee walio na wasiwasi kuhusu kupotezi kazi zao kwa mitambo inayojiendesha.Zaidi ya thuluthi moja ya ajira nchini Uingereza ziko katika hatari ya kuchukuliwa na mitambo ya kujiendesha katika kipindi cha miaka 20 ijayo kulingana na ripoti ya Deloitte.Utafiti huo umebaini kwamba ajira ambazo watu hupata kipato cha chini kuna uwezekano mkubwa zikachukuliwa na mitambo hiyo ya Roboti ikilinganishwa na kazi zinazolipa vizuri.Baadhi ya ajira ambazo ziko katika tishio la kuangamia ni kama vile za usaidizi wa afisi, mauzo na huduma, usafiri, ujenzi, uchimbaji na uzalishaji.