Huwezi kusikiliza tena

Heshima na adabu ya lugha ya Kiswahili

Lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha asilia zinazotumiwa na watu katika mataifa mengi zaidi katika Bara la Afrika.

Kutokana na kuenea kwake, hasa katika Afrika Mashariki na Kati inakisiwa kuwa zaidi ya watu 120 milioni wanazungumza Kiswahili.

Mbali na kuwa na lafudhi mbalimbali kwa sababu ya kuwa katika mataifa tofauti.

Kuna heshima na adabu ya lugha ambayo imeingiliwa na tamaduni ya lugha zingine kama vile Kiingereza.

Muliro Telewa alizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Batilda Buriani anayeanza kwa kueleza heshima na adabu ya lugha ya Kiswahili.