Huwezi kusikiliza tena

Tibaijuka:''Nilipokea pesa za Escrow''

Mjadala kuhusu kashfa ya uchotaji wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya ESCROW ya Benki Kuu ya Tanzania umezidi kuunguruma nchini Tanzania kufuatia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, na ripoti ya serikali kuhusu kashafa hiyo.

Mambo yaliyojitokeza katika ripoti ya PAC ni kutaja majina ya viongozi na maafisa wandamizi wa serikali walionufaika na magao huo.

Miongoni mwao ni waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye alizungumza na mwandishi wetu mjini Dodoma, Ben Mwang'onda ambaye alianza kwa kumuuliza kama kutajwa kwa jina lake alitendewa haki