facebook
Huwezi kusikiliza tena

Facebook yadaiwa kuwaficha magaidi

Kamati ya bunge la Uingereza inayochunguza mauaji ya Fusilier Lee Rigby mwaka uliopita imebaini kwamba kampuni moja ya mtandao nchini Marekani inayodaiwa kuwa facebook inatishiwa kuwa maficho makuu ya magaidi iwapo haitawafichua wateja wake wanaojadili kuhusu harakati za kigaidi.

Mmoja ya watu waliomuua Fusilier,Michael Adebowale anadaiwa kuzungumza kuhusu kumuua mwanajeshi mmoja mapema katika mtandao huo kitu kilichogunduliwa baada ya shambulizi hilo.

Mtandao wa facebook umesema kuwa unakabiliana na itikadi kali.