Huwezi kusikiliza tena

Kenyatta aahidi kupiga Al Shabaab

Rais wa kenya Uhuru Kenyatta amezifanyia mabadiliko nyadhifa za wizara ya usalama wa ndani na ya mkuu wa polisi kufuatia shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa Al shaabab mjini Mandera Kaskazini mashariki mwa Kenya ambapo watu 36 waliuawa

Rais kenyatta alitoa tangazo hilo kwa njia ya runinga kutoka ikulu.

Bwana kenyata aliwataja wale waliofanya mauaji hayo mjini Mandera kwa kuwakata vichwa wasio waislamu kuwa wahalifu wabaya.

Kenyatta amewataka wakenya kuungama katika vita dhidi ya ugaidi.