Huwezi kusikiliza tena

Al Shabaab kero kwa wakenya

Nchi yetu na watu wetu wanashambuliwa" Haya ni maneno ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta---wakati Taifa la Kenya lilipopata taarifa za mauaji mengine ya kikatili kaskazini mwa nchi hiyo.

Wapiganaji wa Al-Shabaab wanasema wamehusika na mauaji ya watu thelathini na sita, wafanyakazi wa machimbo ya mawe huko Mandera.

Rais Kenyatta amemfukuza kazi waziri wa Ulinzi na mkuu wa Polisi amejiuzulu, kama mwandishi wetu Emmanuel Igunza anavyoripoti kutoka Nairobi.