Huwezi kusikiliza tena

Ndoto yageuka biashara kwa mtanzania

Kutana na mwanamke aliyekuwa na ndoto halafu ikatimia.

Mercy Kitomari ana shahada ya biashara na masoko.

Lakini ilikuwa ni kibarua hapa mjini London ambayo ilimvutia na kuanzisha biashara yake nchini Tanzania.

Ameanzisha uzalishaji wake wa malai au ice cream bila kutumia kemikali, katika mji mkuu Dar es Salaam. Anaelezea namna alivyoanzisha biashara hiyo nchini humo mwaka 2012.