Huwezi kusikiliza tena

''Niliponea kifo mikononi mwa Al Shabaab''

Miongoni mwa watu waliowasili katika kuitambua miili ya jamaa zao katika chumba cha kitaifa cha kuhifadhia maiti Nairobi Jumatano alikuwa ni Douglas Ondari Ochodho.

Yeye ni mwalimu wa shule ya upili huko Mandera. Aliponea shambulio la kwanza katika eneo hilo la Mandera wiki mbili zilizopita, ambapo watu takriban 28 waliuawa, miongoni mwao ni mkewe.

Amezungumza na mwandishi wa BBC Maryam Abdallah kuhusu mkosi ulioikumba Safari hiyo.