Huwezi kusikiliza tena

Kampeni za uchaguzi Arusha TZ

Maandalizi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania yamekamilika huku kampeni za vyama na wagombea wao zikipamba moto kwenye maeneo mbalimbali.

Uchaguzi huo utakaofanyika jumapili hii unachukuliwa kama dira ya uelekeo wa uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge nchini humo utakaofanyika mwaka ujao.

Hata hivyo ushiriki wa vijana katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa una umuhimu wake hasa ikizingatiwa vijana wana mahitaji mengi kama vile ajira,elimu,na huduma nyingine muhimu.

Takwimu zinaonyesha kwamba vijana ingawa wanakuwa msitari wa mbele katika kukosoa mambo mbalimbali, lakini ni wachache wanaojitokeza katika kupiga kura.

Hawa hapa ni mashabiki wa chama tawala wakifanya kamepeini zao mjini Arusha.