m23
Huwezi kusikiliza tena

Wapiganaji wa M23 kurudi DRC

Rais wa kundi la waasi wa M23 amesema kuwa wapiganaji zaidi ya mia moja wa kundi hilo walioko nchini Uganda hawajatoroka . Bertrand Bisimwa ameiambia BBC kuwa wapiganaji 1,600 wa M23 wanaoishi katika kambi ya kijeshi nchini Uganda watarejeshwa nyumbani Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo hii leo . Anasema walikimbia kwa kuhofia usalama wa maisha yao nyumbani nchini DRC . Lakini msemaji wa jeshi la Uganda amesema wengi wa wapiganaji hao bado wako chini ya uangalizi wao . Siraj kalyango na taarifa zaidi