The interview
Huwezi kusikiliza tena

Sinema kuhusu Kim Jong Un yazuiliwa

Kampuni ya Sony imefutilia mbali kuonyeshwa kwa filamu kwa jina The Interview ,filamu ya ucheshi kuhusu mauaji ya rais Kim Jong-un .Uamuzi huo unajiri kufuatia vitisho vya kundi moja la wezi wa mitandaoni .Kundi hilo kwa jina Guardian of peace limetishia kushambulia kumbi za sinema nchini Marekani zinazoonyesha filamu hiyo na inadaiwa ni kundi hilo lililofichua makumi ya maelfu ya ujumbe, stakhabadhi na data ilioibwa kutoka kwa kampuni ya Sony Pictures katika kipindi cha majuma kadhaa.