Huwezi kusikiliza tena

Kilio cha wakulima wa Karafuu Pemba

Kisiwa kidogo cha Pemba katika bahari ya Hindi, kilikuwa ndio walimaji wakubwa wa karafuu duniani kwa miaka na mikaka.

Hivi karibuni, nafasi hiyo hivi karibuni imechukuliwa na Indonesia. Wakulima wa karafuu sasa wanasema wanahitaji serikali yao kuwasaidia zaidi ili kuweza kuendeleza kilimo cha zao hilo walilolima kwa miaka mingi.

Karafuu inatumiwa duniani katika chakula, dawa na nchini Indonesia ni moja ya kiungo muhimu kwa utengenezaji wa Cigars.

Salim Kikeke ametutumia taarifa hii kutoka Pemba.