Huwezi kusikiliza tena

Wanariadha wa Kenya hatiani

Wanariadha wawili wa kike nchini Kenya, Viola Kimetto na Joyce Kiplimo, wamepigwa marufuku kushiriki riadha, baada ya Shirikisho la riadha Kenya, kugundua walikuwa wakitumia dawa za kuongezea nguvu.

Wanariadha hao walikuwa wametangazwa washindi wa mbio za nusu marathon mjini Macau, China, mwaka 2013. Shughuli za wanariadha wengine tisa zimesitishwa, kwa kushukiwa pia walitumia dawa za kuongezea nguvu.

Dennis Okari kutoka Nairobi ana maelezo zaidi.