Huwezi kusikiliza tena

Sheria mpya ya usalama Kenya

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametia sahihi sheria mpya ya kukabiliana na maswala ya usalama nchini, ambapo maafisa wa usalama watasikiliza mawasiliano ya simu ya watu hata bila kuwaarifu.

Washukiwa wa uhalifu pia wataweza kuzuiliwa hadi mwaka mmoja bila kufanyiwa mashtaka yo yote.

Rais Kenyatta, ambaye anasema sheria hiyo inahitajika kukabiliana na kundi la kigaidi la Al Shabaab, alisisitiza kuwa haikiuki haki za kibinadamu za mtu ye yote.