Huwezi kusikiliza tena

Polisi watawanya wapinzani Tanzania

Jeshi la Polisi nchini Tanzania jumanne lililazimika kutumia nguvu ili kuwatawanya wafuasi wa upinzani kwa madai ya wafuasi hao kutaka kuvuruga zoezi la kuapisha wenyeviti wa serikali za mitaa wa wilaya Kinondoni lililofanyika mji wa Dar es Saalam.

Wafuasi hao wa upinzani wanadai baadhi ya wenyeviti hao walioapishwa hawakuchaguliwa kihalali na hivyo kuamua kuwaleta watu wengine wanaodai kuwa ndio walioshinda ili nao waapishwe.

Zoezi la kuapishwa wenyeviti hao linafanyika baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika nchini humo mwezi Decemba mwaka jana.

Kutoka Dar es Salaam John Solombi na maelezo zaidi.