Huwezi kusikiliza tena

Imani: Wanyama walemavu huleta laana?

Kwa miaka mingi tumekuwa tukisoma au kusikia kuhusu wanyama ambao wanazaliwa na maumbile yasiyo ya kawaida na yamezua hisia na imani tofauti kutoka kwa makundi tofauti

Kwa jamii fulani, wanyama hao wanakisiwa kuwa na bahati mbaya au laana na kwa wengine ni ishara kuwa jamii hiyo itakumbwa na maafa au janga.

Kwa wengine ni dalili ya mwisho wa dunia na kwa dini zingine ni ishara kutoka kwa mungu kuhusu dhambi za wanazotenda na hivyo wanaichukulia kuwa onyo kuhusu jinsi adhabu yake itakavyokuwa kali.

Wanasayansi nao wanasema ni mabadiliko ya vinasaba au Genes yanayosababishwa na magongwa au mabadiliko ya hali ya hewa. Mwandishi wetu Robert Kiptoo alizuru shamba moja mjini KitaleMagharibi mwa Kenya ambako wanyama hawa wenye ulemavu wanatunzwa