Rekodi ya kusoma kenya
Huwezi kusikiliza tena

Kenya yajaribu kuvunja rekodi ya kusoma

Wanafunzi katika shule 400 nchini Kenya wamesoma hadithi moja kwa pamoja. Zoezi hilo ni jaribio la kuvunja rekodi ya watu wengi zaidi wanaosoma hadithi moja pamoja na kwa sauti. Lengo kuu ni kukuza desturi ya kusoma nchini humo. Mwandishi wa BBC Anne Soy alitembelea shule moja jijini Nairobi kushuhudia walivyosoma.