siku ya saratani duniani
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania yaadhimisha siku ya saratani

Katika kuadhimisha siku ya saratani duniani hospitali ya saratani jijini Dar es salaam nchini Tanzania, imetoa vipimo vya bure kwa Wananchi. Kampeni ya siku ya saratani mwaka wa 2015 Ina kauli mbiu isemayo ugunduzi wa mapema,matibabu kwa wote na kuimarisha hali ya maisha kwa wale wanaouguza. Bara la Afrika limekuwa likikumbwa na vifo vingi vya ugonjwa wa saratani kwa miaka ya karibuni, kwa mujibu wa tathmini ya Taasisi ya saratani ya ocean road ,Tanzania ina wagonjwa wa saratani 100 kwa kila Watu 100,000.Mwandishi wetu, Tulanana Bohela aliitembelea hospitali hiyo na kushuhudia zoezi la upimaji.