Huwezi kusikiliza tena

Congo inawakabili waasi wa FDLR

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimeanza kukabiliana na waasi wa FDLR

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo likisaidiwa na vikosi vya umoja wa Mataifa - vimeanza harakati za kijeshi dhidi ya waasi wa Rwanda wa kundi la FDLR .

Baadhi wa wajiumbe wa kundi hilo wanashutumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda kabla ya kutoroka katika nchi jirani ya Jammuhuri ya kidemokrasi ya kongo , ambako pia wanashutumiwa kutekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, yakiwemo mauaji, ubakaji na uporaji.

Lakini katika kipindi cha wiki moja baada ya kuanza kwa operesheni kubwa ya kukabiliana na kundi hilo , hakuna kinachoendelea , na inavyoelekea hakuna yoyote mwenye haja ya kushambulia waasi hawa.

Mwandishi wa BBC Maud Jullien alikwenda kukutana na waasi wa FDLR katika kijiji kisichoweza kufikiwa kwa urahisi Mashariki mwa DRC .