Uko tayari kutoa kiungo chako kwa mwenzio ?
Huwezi kusikiliza tena

Uko tayari kutoa kiungo chako kwa mwenzio?

Wagonjwa wengi wenye kuhitaji kupata viungo vya mwili kutoka kwa wafadhili nchini Kenya na kwengineko barani Afrika, mara nyingi hulazimika kwenda nje ya nchi ili kufanyiwa upasuaji huo.

Hii imesbabisha hospitali kadha barani kufanya juhudi za kuleta huduma hizo karibu na nyumbani.

Changamoto ni kwamba waafrika wengi bado hawana niya ya kutoa viungo vya miili yao ili kusaidia watu wengine hasa kutokana na sababu za ki mila na kidini.

Mwandishi wetu Anne Soy ametembelea hospitali moja ya macho mjini Nairobi na kutuandalia taarifa hii.