Huwezi kusikiliza tena

Marekani kukabiliana na Boko Haram

Marekani inasema inatafuta njia za kujihusisha zaidi katika vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria.

Naibu kamanda wa wanajeshi wa Marekani barani Afrika, luteni jenerali Stephen Hummer anasema tayari Marekani inashirikiana na Nigeria katika kutoa ripoti za ujasusi katika vita hivyo.

Kamanda huyo alikuwa akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya vikosi hivyo nchini Ujerumani, akama anavyoarifu mwandishi wetu Emmanuel Igunza.