Wanaharakati wawahamasisha wenzao kugombea nafasi za juu za uongozi DRC
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake DRC: watakiwa kugombea uongozi

Image caption wanawake wa DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanawake wanaharakati wamejitokeza kuwaelimisha wanawake wenzao, kujitokeza kugombea nafasi za juu katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo badala ya nafasi hizo kuwaachiwa wanaume peke yao.

Mwandishi wetu Byobe Malenga alihudhuria kampeni za kuwahamasisha wanawake mashariki mwa Congo, na kuzungumza na baadhi ya wanawake kuhusu mtazamo wao katika uchaguzi.