Kanisa la Anglicann nchini Uganda lamkumbuka Askofu Janan Luwum
Huwezi kusikiliza tena

Askofu Janani Jakaliya Luwum akumbukwa

Image caption Kanisa

Wiki hii Uganda inakumbuka kifo cha Askofu mkuu wa zamani wa Kanisa la Kianglikana nchini humo, Janani Jakaliya Luwum.

Janan Luwum aliuawa mwaka 1977 na utawala wa Idi Amin ambao ulidai kuwa alifariki dunia katika ajali ya gari. Bado kuna utata iwapo aliuawa au alikufa kwa ajali na pia tarehe kamili ya kifo chake.

Ingawa vyanzo fulani vya habari nchini Uganda zinasema aliuawa tarehe 16 Februari, lakini Kanisha la Kiprotestanti nchini Uingereza linakumbuka tarehe 17 Febuari kama siku aliyouawa.

Mwandishi wetu wa Kampala Siraj Kalyango amezungumza na mpwa wa marehemu MAGAN ADILE na kuanza kwa kueleza jinsi alivyopokea habari za kifo cha Luwum.