Huwezi kusikiliza tena

Aliyewalawiti Watoto Kenya kuhukumiwa

Raia wa Uingereza aliyewadhalilisha kingono watoto wa kiume katika mji mdogo wa Gilgil nchini Kenya anatarajiwa kuhukumiwa leo nchini Uingereza.

Hii ni baada ya Mahakama ya Birmingham kumkuta na hatia ya kuwadhalilisha watoto wa kiume kingono na pia kupatikana na picha za utupu za watoto.

Simon Harris mwenye umri wa miaka 55 ambaye alikuwa akiendesha Mradi wa misaada kwa Jamii anaaminika kufanya maovu hayo kwa karibu miaka ishirini.

Gladys Njoroge amekutana na baadhi ya waathirika ambao waliomba majina yao yahifadhiwe.