Huwezi kusikiliza tena

Utalii wazorota Pwani ya Kenya

Licha ya msimu wa baridi kali Ulaya inavyoelekea idadi kubwa ya watalii bado wamesusia pwani ya Kenya ambayo walikua wakipendelea kuitembelea hapo miaka ya nyuma.

Hali hiyo inazidi kuathiri wafanya biashara wanaotegemea sekta ya Utalii kujikimu kimaisha.

Wengi wa watalii wa Ulaya wametii amri za mataifa yao kutozuru baadhi ya sehemu za Kenya ikiwemo eneo la Pwani

kutokana na mashambulio ya mara kwa mara ya wanamgambo wa Al Shabaab kutoka Somalia hasa mwaka jana.

Sababu nyingine ya upungufu wa watalii pwani ya Kenya ni ghasia zinazotokana na makabiliano baina ya polisi na waumini wa dini ya kiislamu wanaolalamikia mauaji ya kiholela wanayodai yanawalenga viongozi

wao.

John Nene amezungumza na baadhi ya wafanya biashara mjini Mombasa na kutuandalia ripoti ifuatayo