Kanisa Katoliki lapinga muhula wa 3 Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Kanisa Katoliki lapinga muhula wa 3 Burundi

Nchini Burundi, kanisa katoliki lenye waumini zaidi ya asilimia 80 ya wananchi limeweka wazi msimamo wake kwamba rais wa sasa hawezi kuwania muhula wa tatu kulingana na mkataba wa amani wa Arusha.

Shinikizo hilo la kanisa katoliki linajitokeza baada ya Muungano wa Jumuiya ya Ulaya na Marekani kumuonya Rais Pierre Nkurunziza kutowania muhula mwingine, hali ambayo inaweza kutishia utengamano wa taifa hilo lililopitia vita

vya zaidi ya Muongo mzima .

Kutoka Bujumbura, Muandishi wetu Ramadhani Kibuga anaarifu zaidi.