Wanawake walivyoathirika na dawa za kulevya Zanzibar
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake waathiriwa na mihadarati TZ

Dawa za kulevya zinaendelea kuwa tatizo sehemu mbalimbali duniani.

Imeelezwa kuwa utumiaji wa dawa hizo miongoni mwa wanawake ni changamoto kubwa katika jamii, kutokana na athari zake kujiitokeza kwa haraka zaidi katika familia.

Kwa mujibu wa tume ya taifa ya kuratibu na kudhibiti dawa za kulevya Zanzibar, wanawake ndio walezi wakuu wa familia na wanapopata tatizo hilo, huwezi kutarajia kupata kizazi kilicho bora.

Halima Nyanza alitembelea moja ya nyumba ya kurekebishia tabia visiwani Zanzibar na kuzungumza na wasichana walioko kwenye tiba hiyo.