Huwezi kusikiliza tena

Lahaja za Kiswahili

Image caption Lahaja ya Kitumbatu ikijadiliwa

Lugha ya Kiswahili ina Lahaja kadhaa kama vile Kiamu kinachozungumzwa Lamu, Kimvita(Mombasa), Kibajuni huzungumzwa sehemu za Kismayu, Somalia, Kipemba, Kitumbatu na Kimakunduchi huzungumzwa Zanzibar. Halima nyanza alitembelea visiwani Zanzibar, kujua zaidi juu ya Lahaja hizo zilivyoweza kuwa hai mpaka sasa, licha ya matumizi makubwa ya kiswahili sanifu.