Matumizi ya lugha ya Kiswahili  kufundisha kuanzia shule za upili na kuendelea juu
Huwezi kusikiliza tena

Matumizi ya Kiswahili kufundisha Tanzania

Mwezi uliopita, Tanzania ilitangaza mipango mipya ya kuimarisha upya mfumo wa elimu.

Muhimu zaidi, ni kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundisha kuanzia shule za upili na kuendelea juu.

Kwa miaka mingi, shule za upili na vyuo nchini humo vimetumia Kiingereza.

Lakini je, hatua hiyo ya serikali itafaa au la?

Mwenzangu Salim Kikeke alizungumza na mwalimu na mwanafunzi wa shule ya Minaki, kutoka Tanzania, ambao walitembelea studio za, London.