Msanii wa nyimbo za injili  Kenya Papa Denis  amesifu huduma mpya ya mtandao wa muziki wa Tidal uliozinduliwa na Jay Z.
Huwezi kusikiliza tena

Papa Denis asifu mtandao wa Jay Z Tidal

Image caption Dennis Mwangi ama Papa Denis ni msanii wa injili nchini Kenya.

Baadhi ya majina makubwa katika fani ya burudani wamezindua upya huduma ya usajili wa miziki yao - Tidal,

ambapo wanatoza malipo kadri msanii anavyotoa muziki ama video .

Huko New York, Madonna, Rihanna, Beyonce and Alicia Keys walikua miongoni mwa wanamuziki waliotangaza kuwa watashirikiana umiliki katika Tidal,

ambayo ilianza kuchezwa mwezi Oktoba mwaka jana na pia kununuliwa na nyota wengine wa muziki Jay Z.

Tidal ni mshindani wa moja kwa moja wa Spotify, ambayo huwapatia watumiaji huduma kama hiyo.

Dennis Mwangi ama Papa Denis ni msanii wa injili nchini Kenya.

Anaelezea jinsi mtandao waTidal unavyoweza kuwasaidia wasanii kuuza muziki wao tofauti na hali ilivyo kwa wasanii Kenya .