CAR:Seleka na anti -Balaka zakubaliana

Pande mbili zinazozozana katika Jamhuri ya Afrika ya Kati zimefikia makubaliano ya amani ya kudumu baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Nairobi nchini Kenya.

Makubaliano hayo muhimu yametiwa sahihi na mwakilishi wa kundi la wapiganaji wa kikristo Anti Balaka Joachim Kokate

na muwakilishi wa kundi la waasi wa Seleka aliyekuwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Mitchel Djotodia.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto walishuhudia makubaliano hayo kati ya makundi hasimu ya seleka na anti balaka katika ikulu ya Nairobi .