Raia wa kigeni akiadhibiwa na mwenyeji wa Afrika Kusini,ati kwa kuchukua ajira za wenyeji.
Huwezi kusikiliza tena

Durban wageni! hamkani si shwari.

Afrika Kusini inakumbwa na wakati mgumu kutokana na kukithiri kwa visa vya mashambulizi dhidi ya wahamiaji na wageni wa Kiafrika, katika baadhi ya miji yake. Hadi sasa watu watano wameuawa kwenye mashambulio hayo. Baadhi ya nchi ikiwemo Malawi na Somalia zinapanga jinsi ya kuwaondoa raia wake mkutoka Afrika Kusini. Taarifa za hivi karibuni zinasema kumetokea mashambulio mengine eneo la Durban.

Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amezungumza na mkaazi wa Durban,ABEDI JEAN DELA CROIX maarufu sana JAY-C, ambaye ni Raia wa DRC anayeishi DURBAN afrika kusini.