Agathon Rwasa wa chama cha UPRONA akihutumia nyuma ya askari,Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Francois Bizimana aachiliwa huru

Watu wawili waliuawa katika siku ya kwanza ya maandamano ya upinzani nchini Burundi .Watu hao walipigwa risasi na polisi wakati wa maandamano hayo mjini Bujumbura.

Wafuai hao wa upinzani wanatarajiwa kuendelea na maandamano hayo, kujaribu kumshurutisha rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kubadili uamuzi wake wa kuwania muhula mwingine.

Ulinzi umeimarisha katika sehemu nyingi za burundi huku raia wengine wakikimbilia nchi jirani kuhofia machafuko zaidi.

Wakati huo huo habari kutoka Bujumbura zinasema kuwa aliyekuwa wakati mmoja Mjumbe wa Burundi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Francois Bizimana, aliyetekwa nyara hiyo jana ameachiwa huru. Kufuatia hali hiyo mwandishi wa BBC kutoka mjini Dar-Es-salaam,Regina Mziwanda amezungumza na Agathon Rwasa wa chama cha upinzani cha FNL ,kutaka kujua hali ya mambo nchini Burundi kuelekea kwenye uchaguzi ambao tayari una mazonge ya kutokubalika kwa uamuzi wa rais aliyeko madarakani kugombea muhula mwingine.