Hifadhi ya wanyama pori ya Entebbe nchini Uganda yapata simba dume mpya
Huwezi kusikiliza tena

Hifadhi ya wanyama yapata simba mpya UG

Tangu Kibonge-Simba dume pekee katika hifadhi ya wanyama ya Entebbe maarufu kama Zoo afariki miezi kadhaa iliopita simba wa kike watatu waliomo kwenye hifadhi hiyo walibaki bila dume hadi juzi ambapo zoo hiyo ilipata dume jingine kutoka Afrika Kusini.

Simba mpya anaitwa Letaba. Mwandishi wetu Siraj Kalyango alikwenda katika hifadhi hiyo na kumuona Simba huyo mgeni na kutuandalia taarifa ifuayo.