Huenda kuanza kwa muhula wa pili wa kalenda ya elimu nchini Kenya ukatatizika kaunti ya Garissa.
Huwezi kusikiliza tena

Mashambulizi yaathiri elimu Garissa

Nchini Kenya, hofu imetanda kwenye sekta ya elimu katika mji wa Garissa kaskazini mashariki mwa taifa hilo kutokana na ukosefu wa usalama unaosababishwa na mashambulizi ya kigaidi. Tayari chuo kikuu cha Garissa kimefungwa kwa muda usiojulikana baada ya mauaji ya watu 150 wengi wao wanafunzi mwezi mmoja uliopita. Na kama anavyoripoti mwandishi wa BBC Wanyama wa Chebusiri ambaye amekuwa mjini Garissa, huenda kuanza kwa mhula wa pili wa kalenda ya elimu nchini Kenya ukatatizika.