Watu watatu wadaiwa kuuawa katika maandamano nchini Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Watu 3 wauawa katika maandamano Burundi

Watu watatu wamefariki kwenye makabiliano baina ya Polisi na waandamanaji mjini Bujumbura Burundi, huku wananchi wakiendelea kuelezea pingamizi zao kuhusu uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu kama Rais wa nchi hiyo. Kutokana na hali ilivyo nchini Burundi zaidi ya raia wake elfu mbili wamepokelewa nchini Tanzania kama wakimbizi tangu siku ya Jumapili. Mbali na watu wawili waliouawa kwenye ghasia za leo mjini Bujumbura, shirika la msalaba mwekundu linasema raia 45 wamejeruhiwa, na pia maafisa Polisi 17. Mwenzetu Robert Kiptoo ana maelezo zaidi.