Huwezi kusikiliza tena

Waingereza kupiga kura

Alhamis Mei 7 wananchi hapa Uigereza wanapiga kura kwenye uchaguzi mkuu, ambao ni dhahiri utakuwa tofauti kabisa na uchaguzi uliowahi kufanyika katika nchi hii. Viongozi wa vyama vikuu wamekuwa wanaendesha kampeni katika mkesha wa uchaguzi huo. Kutokana na umaarufu wa vyama vidogo pamoja na jaribio la Scotland la kutaka kuwa huru, mpaka sasa hakuna chama kikubwa ambacho kina uhakika wa kupata ushindi wa kuweza kudhibiti bunge.Peter Musembi ameandaa ripoti hii.