Masaibu ya wakimbizi Sudan Kusini
Huwezi kusikiliza tena

Masaibu ya wakimbizi Sudan Kusini

Kila siku watu takriban elfu thelathini wanatoroka makwao wakikimbia vita na vurugu.

Umoja wa Mataifa unasema idadi hiyo imetokana na ongezeko la mizozo hasa katika mataifa manne - Syria, Iraq, Ukraine, na Sudan Kusini.

Mkataba wa amani Sudan Kusini haujatekelezwa huku maelfu wakiendelea kuumia.

Mwandishi wetu Emmanuel Igunza ametembelea kambi moja ya wakimbizi kwenye jimbo la Jonglei na kuona hali ilivyo.