Marais Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo jijini Dar Es Salaam kujadili mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi.
Huwezi kusikiliza tena

Mazungumzo ya kutafuta amani Burundi

Marais Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo jijini Dar Es Salaam kujadili mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi.

Mkutano huo utakuwa chini uenyekiti wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, aliyeuitisha baada ya ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jumuiya hiyo, kwenda Bujumbura wiki iliyopita.

Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi wenzake.

Benard Membe ni waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, ambao ndiyo wenyeji wa mkutano huo.